Tunamuombea Rais mteule kwa Mwenyezi Mungu, ampe afya njema, ujasiri na hekima, na amsimamie katika jukumu lake kubwa la kuongoza Watanzania kwa amani, utulivu na ustawi wa taifa.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameapishwa rasmi jana, tarehe 03 Novemba 2025, kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, akianza rasmi kipindi chake cha pili cha uongozi katika awamu ya sita ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hafla hiyo adhimu imefanyika katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino, Jijini Dodoma, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mataifa ya Afrika na nje ya Afrika, pamoja na wakuu wa mashirika ya kimataifa, mabalozi, viongozi wa dini na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Katika hotuba yake ya baada ya kuapishwa, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alisisitiza dhamira yake ya kuendeleza amani, umoja, na maendeleo jumuishi kwa Watanzania wote, huku akiahidi kuimarisha uchumi, elimu, afya na miundombinu kwa manufaa ya taifa.

Tunamuombea Rais mteule kwa Mwenyezi Mungu, ampe afya njema, ujasiri na hekima, na amsimamie katika jukumu lake kubwa la kuongoza Watanzania kwa amani, utulivu na ustawi wa taifa.

Your Comment